Dhamira Yetu
NIRUDI ina dhamira ya kuwaunganisha wakulima, wazalishaji na wasambazaji na wanunuzi pamoja na walaji kwa njia rahisi na yenye ufanisi. NIRUDI hukusanya, kuainisha na kutoa taarifa za kiwango cha kimataifa kuhusu bidhaa na huduma. NIRUDI inamwezesha mtu yeyote, wakiwemo watu binafsi, kampuni ndogo na za kati, pamoja na mashirika, kutoa taarifa, kuonyesha, kuomba, kutoa ofa na kuuza bidhaa na huduma kwa urahisi kutoka mahali popote duniani, wakati wowote na kupitia kifaa chochote kilichounganishwa na intaneti.